Bora kwa msafiri ni kuswali kwa kufupisha

Swali: Nilitoka ar-Riyaadh wakati ambapo kulikuwa kunaadhiniwa maghrib nikielekea mji wa nje. Nikachelewesha maghrib mpaka wakati wa ´ishaa na nikaikusanya pamoja na ´ishaa pasi na kufupisha. Je, ni sahihi?

Jibu: Ndio, hakuna neno. Kinachozingatiwa ni kile alichofanya. Kukiadhiniwa na wewe bado uko ndani ya mji halafu usiswali mpaka ulipoanza safari hakuna neno. Lakini lililokuwa bora ni kufupisha. Swali maghrib Rakaa´ tatu na ´ishaa mbili.

Wako wanachuoni ambao wanasema haijuzu kuswali kikamilifu safarini. Lakini maoni ya sawa ni kwamba inajuzu. Dalili ya hilo ni kwamba ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) alisafiri katika hajj na Maswahabah wakaswali nyuma yake kikamilifu. Ni dalili inayoonyesha kujuzu. Lakini hata hivyo bora ni kufupisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 07/07/2018