Bora kwa msafiri kufunga na kuswali kikamilifu au kula na kufupisha?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na kufunga safarini? Je, kuswali kikamilifu na kufunga ndio bora au lililo bora ni kuchukua ruhusa za Kishari´ah pamoja na kujua kuwa umbali hii leo umekuwa karibu na hakuna ugumu wowote  katika safari?

Jibu: Inajuzu kwa msafiri kula katika Ramadhaan na kufupisha swalah za Rak´ah nne. Hilo ni bora kuliko kufunga na kuswali kikamilifu. Hayo ni kutokana na yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Hakika Allaah anapenda zitendewe kazi ruhusa Zake kama anavyochukia kuendewa maasi Yake.”[1]

Amesema vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Sio katika wema kufunga safarini.”[2]

[1] Ahmad (02/18).

[2] Muslim (02/786), Ahmad (03/299), Abu Daawuud (02/796) na wengineo

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/200)
  • Imechapishwa: 06/06/2017