Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia mswaki na dawa ya meno baada ya kuingia alfajiri?

Jibu: Hakuna neno kwa mfungaji kutumia mswaki na dawa ya meno. Lakini kutokana na ile nguvu ya dawa ya meno bora mtu asiitumie hali ya kuwa amefunga. Kwa sababu huteremka kooni na tumboni bila ya mtu kuhisi hilo. Hakuna dharurah inayopelekea kufanya hivo. Kwa hivyo mtu ajiepushe mpaka pale atapokata swawm. Badala yake afanye hivo usiku na isiwe mchana. Lakini hata hivyo kimsingi ni kwamba inajuzu na hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/355)
  • Imechapishwa: 10/06/2017