Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Tasbihi wakati wa kufanya Adhkaar?

Jibu: Kutumia Tasbihi inafaa. Lakini bora ni kuleta Adhkaar kwa vidole. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hesabuni kwa vidole. Kwani hakika vitazungumzishwa.”[1]

[1] Ahmad (06/370), Abu Daawuud (1501) na at-Tirmidhiy (3583) ambaye yeye upokezi wake unasema:

“Hesabuni kwa vidole. Kwani hakika vitaulizwa na vitazungumzishwa.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 336
  • Imechapishwa: 09/05/2020