Swali: Mwanafunzi ambaye anatengana na familia yake kwa sababu ya kutafuta elimu, je, kitendo hicho kinazidi kumkurubisha mbele ya Allaah? Tunatarajia utatutajia baadhi ya fadhilah kuhusu kujifunza elimu ambazo zimepokelewa katika Qur-aan na Sunnah ambazo zinatushaji´isha na kutufanya kuzidi kujifunza elimu?

Jibu: Hapana shaka kwamba kule mwanafunzi kutafuta elimu hata katika miji mingine kisha akahama kwa ajili ya kutafuta elimu kwamba yeye ni mbora kuliko yule ambaye anatafuta elimu katika mji wake. Hapa ni pale ambapo nia zao za kusoma na aina ya elimu vitakuwa ni vyenye kulingana. Kwa sababu huyu ameicha nchi yake, familia yake na yale aliyokwishazowea kwa ajili tu ya kujifunza elimu. Hivyo huyu ndiye mbora zaidi. Kama ambavyo mara nyingi yule anayesafiri kwa ajili ya kutafuta elimu anakuwa na wakati mwingine wa faragha kuliko yule ambaye anatafuta elimu katika nchi yake. Kwa sababu katika nchi yake mara nyingi anashughulishwa na familia yake kutokana na mahitajio yao na mengineyo na hivyo akawa ni mwenye kupitwa na kheri nyingi. Jengine ni kwamba mara nyingi mwanafunzi anayesafiri kwa ajili ya kutafuta elimu anakutana na watu asiowapata katika nchi yake. Mara nyingi marafiki wa nchi moja wanampumbaza mtu. Upande mwingine marafiki ambao hawatoki nchi moja na mtu – maadamu wote wamekuja kwa ajili ya kutafuta elimu – humsaidia juu ya kujifunza elimu. Kuhusu maombi yake kutaja fadhilah za kujifunza elimu ni mambo yametajwa kwenye vitabu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (67) http://binothaimeen.net/content/1515
  • Imechapishwa: 11/02/2020