Swali: Lililo bora ni kusoma Qur-aan usiku au mtu alale na kuisoma mchana baada ya swalah mbalimbali?

Jibu: Asome kwa kiasi na vile itavyomkuwia wepesi kwake sawa iwe usiku au mchana. Lakini hata hivyo kusoma usiku ndio bora zaidi. Kwa kuwa Jibriyl (?alayhis-Salaam) alikuwa akimfunza Mtume (Swalla Allaahu ?alayhi wa sallam) Qur-aan usiku. Kwa hivyo kisomo cha usiku ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 28/05/2017