Swali: Kuna ndugu katika Salafiyyuun amemposa dada ambaye anasoma katika mazingira ya mchanganyiko wa wanaume na wanawake. Alimnasihi, lakini akakataa. Unamnasihi nini kijana?

Jibu: Nanmasihi kwa nasaha ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Mchague mwanamke wa dini.”

Tafuta mwanamke wa dini hata kama atakuwa sio msomi. Mwanamke ambaye si msomi ni bora kuliko mwanamke msomi mwenye kusoma katika mazingira ya mchanganyiko. Leo wanawake wengi ambao sio wasomi ni bora na ni wenye akili kuliko wanawake wasomi. Sio lazima kuoa mwanamke msomi. Badala yake kuchukua mwanamke ambaye ni mchaji Allaah na ambaye ni mwema. Aidha awe ni msomi, jambo ambalo ni nzuri tu, au sio msomi pamoja na kuwa na mwelekeo wa asili; unamchukua na kumfunza na yeye anapokea hayo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy.
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ash-Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy (2/418)
  • Imechapishwa: 22/09/2020