Bora hifadhi pesa mahali ambapo hazitumiwi katika ribaa

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka pesa katika benki ya ribaa bila kuchukua faida?

Jibu: Akihitajia kufanya hivo kwa sababu ya haja hakuna neno. Midhali hachukui faida ni sawa. Lakini lililo bora ni yeye azihifadhi sehemu ambayo yule mwenye nazo hazitumii katika ribaa. Lakini hata hivyo azihitajia kufanya hivo kutokana na dharurah hakuna neno. Kwa sharti asichukue ile faida.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 11/03/2018