Binti mwasherati wa mchungaji


7Kwa kuwa mchungaji amewekwa wakfu kwa Mungu wake, kamwe asioe kahaba, wala mwanamke asiye bikira wala aliyepewa talaka. 8Utamtambua mchungaji kuwa aliyewekwa wakfu, maana yeye ndiye anayetoa sadaka ya mkate wa Mungu wako; utamtambua kuwa mtakatifu, maana mimi Mwenyezi-Mungu ninayekuweka wewe wakfu, ni mtakatifu. 9Binti wa mchungaji yeyote akijitia unajisi kwa kufanya ukahaba, atateketezwa kwa moto kwani anamtia baba yake unajisi.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Walawi 21:07
  • Imechapishwa: 12/01/2020