Binti mdogo hatakiwi kuolewa kabla ya yule binti mkubwa kuolewa


Swali: Je, ni lazima kwa baba kumzuia binti mdogo kuolewa mpaka pale ambapo binti mkubwa ataolewa?

Jibu: Haijuzu kwa baba kumzuia binti mdogo kuolewa ikiwa kuna mtu ambaye kamchumbia kwa sababu tu binti mkubwa hajaolewa. Hili ni katika mila za wajinga ambazo zinakosa mashiko katika Shari´ah. Wanafikiria kuwa hili linamdhuru yule mkubwa ikiwa yule mdogo ataolewa kabla yake. Ikiwa ni hivyo kweli, basi hili linamdhuru vilevile hata yule binti mdogo – na kanuni inasema:

“Madhara hayaondolewi kwa madhara mengine.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Muntaqaa (3/152)
  • Imechapishwa: 20/09/2020