Swali: Dada huyu anasema. Sisi ni kongamano la wajane. Tunataka uwashauri wasimamizi wetu miongoni mwa mababa na kaka kukimbilia kuwaozesha wasichana wao na dada zao na kutochelewesha mpaka anapokuja wa kumchumbia. Na nyinyi mnajua fika ya kwamba binti ni mwenye kuona haya kusema nataka kuozeshwa kama jinsi alivyo mvulana.

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ

“Waozesheni wajane miongoni mwenu… “ (24:32)

(الْأَيَامَىٰ) maana yake ni wale ambao hawajaoa na kuolewa katika wavulana na wasichana. Yule ambaye hana mume au mwanamke ambaye hana mume. Ni wajibu kwa msimamizi wake ajitahidi kumtafutia binti yake mume mzuri. Akichumbiwa akimbilie kuitikia. Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atapokujieni yule mnayemridhia dini yake na amana yake basi muozesheni. Msipofanya hivyo, itakuwa fitina katika ardhi na ufisadi mkubwa.”

Ikiwa hajachumbiwa, walii yeye mwenyewe mtafutie na kumchagulia binti yake. Kwa kuwa yeye ndiye mas-uul kwa binti huyu. Amtafutie mwanaume mwema hata kama yeye ndiye atamwendea amuombe kumuoa binti yake au dada yake ili asije kupotea na ujane wake kisha wanaume wakaja kutoka nae na akabaki hali ni muulizwaji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–1428-03-01.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020