Bima za gari, za afya, za bidhaa na za uhai zote ni udanganyifu

Swali: Kuna sura ipi ya bima inayofaa?

Jibu: Sijui sura ya bima inayofaa. Isipokuwa tu ile bima inayoitwa “bima ya kusaidiana”[1]. Nayo ni ile ambayo kundi la watu likakusanyika na wakakubaliana kila mmoja wao kutoa kiwango fulani cha pesa na kinapokea mmoja katika wao. Kitendo hichi hakina neno.

Kuhusu bima za uhai, bima za gari, bima za bidhaa na bima za afya ni udanganyifu. Fatwa zinasema kuwa ni haramu. Kwa sababu ni katika mambo ya udanganyifu na ni kula mali kwa njia ya batili. Jengine ni kwa sababu moja katika mashirika yanapata faida na huku mengine yanapata khasara. Anaweza kuitolea bima gari yake ambapo akashtushwa na kulazimishwa kutoa kiwango kikubwa zaidi ya thamani yake. Isitoshe anaweza kuitumia gari yake miaka na kila mwezi akalipa malipo na wala hanufaiki kwayo kwa lolote. Ni kipi kinachomhalalishia kuchukua mali hii kwa kuitengenezesha gari yake kwa njia ya batili?

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ibn-uthaymiyn-kuhusu-kucheza-kikoba-kibati/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191634
  • Imechapishwa: 22/03/2020