Swali: Je, katika dini kuna Bid´ah nzuri?

Jibu: Kuna watu wenye kuonelea hivi ya kwamba katika dini kuna Bid´ah nzuri na mbaya. Sahihi ni kwamba katika dini hakuna Bid´ah yoyote nzuri.  Dalili ya hilo ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila Bid´ah ni upotevu.”

Katika “as-Sunan” ya an-Nasaa´iy imekuja:

“Kila upotevu ni Motoni.”

Vilevile ameema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”

Sahihi ni kwamba Bid´ah zote ni upotevu. Hakuna ambayo ni nzuri. Bid´ah zote ni mbaya.

Kuhusu yale baadhi ya watu wanayofikiria kuwa yanaingia katika Bid´ah sio katika Bid´ah. Mambo hayo yanaweza kuwa yanaingia katika mambo ya manufaa yaliyoachiwa. Kama mfano wa ukusanyaji wa Qur-aan. Kitendo cha Abu Bakr kukusanya Qur-aan kuna wanaosema kuwa ni katika Bid´ah nzuri. Uhakika wa mambo sivyo hivyo. Ni katika mambo ya manufaa yaliyoachiwa. Kuhusu Bid´ah zote ni mbaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Kila Bid´ah ni upotevu.”

Katika “as-Sunan” ya an-Nasaa´iy imekuja:

“Kila upotevu ni Motoni.”

Kwa hivyo Bid´ah zote ni mbaya. Bid´ah ni kule kuzua katika dini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=67930&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 29/07/2017