Swali: Msemo unaosema kuwa Ahl-ul-Bid´ah ni waovu zaidi kuliko watenda maasi hautakiwi kuchukuliwa kama ilivyo ni sahihi?

Jibu: Hapana, si sahihi. Bid´ah ni shari zaidi kuliko maasi. Haijalishi kitu ni Bid´ah aina gani. Kwa sababu mtenda madhambi anajua kuwa ni mwenye kukosea na kunatarajiwa kuwa atatubu. Upande mwingine mtu wa Bid´ah yeye anaona kuwa yuko katika haki na haoni kuwa ni mwenye kutenda maasi na hatubu. Ni mara chache sana mzushi kutubu. Bid´ah ni shari zaidi kuliko madhambi. Bid´ah ni yenye kupendwa zaidi kwa Ibliys kuliko madhambi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14725
  • Imechapishwa: 03/05/2018