Swali: Nimetoa Khutbah kuhusu kuwatendea wema wazazi. Je, ni sawa kwangu kusoma Aayah ambazo zinaonesha uwajibu wa kuwatendea wema wakati wa Swalah?

Jibu: Hapana. Usifanye kisomo cha Swalah kikawa kinahusiana na maudhui ya Khutbah. Hili ni jambo limezushwa na baadhi ya vijana. Usifanye kisomo cha Swalah kikawa kinahusiana na maudhui ya Khutbah. Ukiwa na wepesi Aayah hizo zisome wakati wa Khutbah na sio wakati wa Swalah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-5-29.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014