Swali: Bibi yangu alikuwa haswali kutokana na uzembe na uvivu. Lakini alikuwa mwenye kumuamini Allaah na Mtume wake. Je, inafaa kwangu kumtakia rehema na kumfanyia ´Umrah?

Jibu: Hapana, yule ambaye haswali na wakati huohuo yuko na akili yake, kumbukumbu zake lakini akaacha swalah si muislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliopo kati yetu na wao ni swalah. Hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18252
  • Imechapishwa: 17/07/2020