Biashara ya sigara na mavazi na nepi zilizo na picha

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuuza sigara na nguo zilizo na picha? Je, biashara hii inafaa? Kile anachochuma ni halali au haramu?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kuuza sigara. Sigara ni haramu. Allaah akiharamisha kitu basi anaharamisha vilevile thamani yake. Jengine ni kwa sababu kule kuuza ni kusaidia katika dhambi na uadui.

Kadhalika haijuzu kuuza mavazi yaliyo na picha nzima. Biashara hii inapelekea zikavaliwa na kuzivaa ni haramu. Ama picha ikiwa iko na uso peke yake sio haramu.

Vivyo hivyo nepi zilizo na picha. Hakuna ubaya kufanya biashara ya vitu kama hivi kwa sababu picha hizi zinatwezwa vibaya sana kwa kule kuwekwa sehemu chafu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1303
  • Imechapishwa: 21/10/2019