Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu juu ya biashara ya misahafu?

Jibu: Madhehebu [ya Hanaabilah] wanasema kuwa haijuzu kufanya biashara ya misahafu. Lakini maoni yenye nguvu – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba inafaa kuifanya. Waislamu daima ni wenye kuuziana misahafu tokea kipindi cha Maswahabah. Jengine ni kwamba ikiachwa kuuzwa basi itafutika na upatikanaji wake utakosekana kwa watu. Kwa hivyo hakuna neno kufanya biashara ya misahafu. Uuzaji unatokana na ile kazi ya mtu kama vile makaratasi, ngozi, uandishi n.k.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 18/04/2021