Swali: Biashara ya nyani na punda inaweza kulinganishwa na biashara ya mbwa ambapo chumo linalotokamana na biashara hiyo ikawa chafu?

Jibu: Inafaa kuuza punda. Walikuwa wakiuziana punda katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَالْخَيْلَ وَالْبِغَالَ وَالْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ

”Farasi na nyumbu na punda ili muwapande na wawe mapambo – na Anaumba msivyovijua.”[1]

Kwa hivyo inafaa kuuza punda. Kuhusu ngedere haijuzu kuuza; nyani ni chafu zaidi kuliko mbwa.

[1] 16:08

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (26)
  • Imechapishwa: 11/05/2021