Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya biashara wa ndege wenye kuimba?
Jibu: Haina neno wakiwa ni wale ndege walioruhusiwa, kama vile majogoo, kuku na wengineo. Hata hivyo haijuzu kufanya biashara wa ndege ambao hawakuruhusiwa kama mfano wa tai na kipanga.
Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya biashara wa samaki wa mapambo wanaoweka kwenye matenki ya vio vya maji kwa ajili ya kuwaangalia?
Jibu: Ikiwa jambo hilo ni la kawaida kati ya watu, haina neno.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
- Imechapishwa: 05/02/2022