Swali: Kumetokea tofauti kuhusu biashara ya mirungi juu ya kufaa na kutokufaa. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Kinachozingatiwa sio tofauti; kinachozingatiwa ni dalili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuuza vitu vichafu na vyenye kudhuru. Yote mawili yanapatikana kwenye mirungi; ni yenye kudhuru na vitu vichafu, vyenye kupoza na kulevya. Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kila chenye kulevya na kupoza.”

Kwa ajili hiyo wanaketi na kutafuna kwa muda mrefu na zinawapita mpaka swalah. Wanapitwa na swalah huku wako wanatafuna. Ni chafu na haijuzu. Mirungi ni mbaya zaidi kuliko sigara. Aidha haijalishi kitu ambaye ameonelea  kinyume ambao wanapanda mirungi au mwanafunzi wenye kuhalalisha. Hawazingatiwi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 18/04/2021