Biashara ya kuuza Qur-aan na kanda za mawaidha

Swali: Ni ipi hukumu ya kujichumia riziki kwa kuuza misahafu ya Qur-aan na kanda za Qur-aan?

Jibu: Kanda ni sawa. Kwa sababu kazi yake huuzikana. Inahusiana na kanda na  tafsiri za Qur-aan. Haina maana kwamba mtu anauza ile Qur-aan. Kadhalika misahafu [inafaa]. Ikiwa anakusudia kule kuzichapisha ni sawa. Wanachuoni tokea hapo kale walikuwa wakiruhusu kuuza misahafu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 05/10/2018