Swali: Ninapokuwa msikitini katika darsa hupigiwa simu na baadhi ya wateja wanataka bidhaa fulani. Je, inafaa kwangu kuwajibu ndani ya msikiti?

Jibu: Hapana, haijuzu kufanya biashara ndani ya msikiti. Ni mamoja biashara hiyo ni kwa njia ya simu au njia ya mazungumzo ya mdomo. Hiajuzu kufanya hivo. Haijuzu kufanya biashara wala kukodishiana [ndani ya msikiti].

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 19/04/2021