Benki haikukopi isipokuwa kwa ribaa

Swali: Je, inajuzu kuchukua mkopo wa benki?

Jibu: Mkopo mzuri unajuzu. Mkopo ambao hauna ribaa wala kuwekeza unajuzu; mkopo ambao unakopa kiwango fulani cha pesa na unarudisha hicho hicho bila ya ziada. Huu ndio mkopo mzuri. Ama kuhusiana na mkopo unaotakiwa kutoa ziada au manufaa (hata kama sio ziada) ni ribaa. Kila mkopo wenye kupelekea katika manufaa ni ribaa. Haijalishi kiti ikiwa unachukuliwa kutoka kwenye benki au kwenginepo. Benki haukopi isipokuwa kwa ribaa [faida].

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–02041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015