Inanisikitisha kusema ya kwamba wapotevu kwa sampuli zao zote kutoka katika vipote potevu, madhehebu ya fikra zilizopinda na wengineo wote wanashirikiana katika kuwaponda wanachuoni kwa kutumia mshale mmoja. Wanafanya hivo kwa sababu wao ndio watetezi wa Shari´ah. Pamoja na kuwa wanatofautiana katika matusi yao na uzushi wao. Utawasikia baadhi yao wanasema kuwa wanachuoni ni vibaraka wa wafalme. Wengine wanasema ya kwamba wanachuoni hawaelewi chochote katika mambo ya kisasa. Wengine utawasikia wanasema kuwa wanachuoni ni Murji-ah. Baadhi ya wengine utawasikia wanawatuhumu wanachuoni ya kwamba wanawakufurisha wale wanaowakhalifu, hivyo ndivyo wanavyosema Suufiyyah na Shiy´ah. Kuna mengine yanayosemwa mbali na hayo.

al-Hajuuriy ameafikiana nao kwa kuwatukana wanachuoni kwa matusi mbalimbali[1]. Isipokuwa tu yeye anafanya hivo nyuma ya pazia kwamba anaitetea haki, kama alivyokuwa akifanya khabithi Mahmuud al-Haddaad. Mtu huyu hakuwasalimisha wanachuoni katika wakati wake mpaka wakiwemo Kibaar-ul-´Ulamaa´. Wanachuoni hawakusalimika naye pindi walipotoa fatwa juu ya kufaa kuwataka msaada makafiri katika vita vya pili vya Ghuba. al-Haddaad akasema kuwa ni wanachuoni waovu, kwamba wanasema wasiyoyafanya, kwamba ni watumwa wa serikali, kwamba wanaharamisha vya halali kwa amri ya serikali na wanahalalisha vya halali kwa amri ya serikali na kwamba fataawaa zao ni za maslahi ya kidunia. Hivi ndivyo alivyosema. Allaah amlipe kwa kile anachostahiki.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/mfano-namna-ambavyo-al-hajuuriy-hana-adabu-kwa-maimamu-wa-ahl-us-sunnah/

  • Mhusika: Shaykh Abu ´Ammaar ´Aliy al-Hudhayfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://m-noor.com/showthread.php?p=33728
  • Imechapishwa: 18/02/2017