Swali: Mwanamke mwenye kufanya Ihraam amekatazwa kuvaa Niqaab wakati wa kuhirimia. Je, bado ni lazima kwake kufunika uso wake kikamilifu wakati wa Twawaaf?

Jibu: Hapana shaka. Anatakiwa kufunika uso wake mbele ya wanaume, sawa katika Twawaaf na kwenginepo. Anatakiwa kuufunika na khimari yake au na nguo yake:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako na wanawake wa waumini wajiteremshie Jilbaab zao. Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

[1] 33:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (90) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20-15-07-1439.lite__0_0.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2018