´Uthmaan ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kutambua kuwa hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah basi ataingia Peponi.”[1]

Hadiyth ni geni, amepwekeka nayo Ibn Humraan katika kuisimulia.

Mja hawi mwenye kutambua ya kwamba ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah` mpaka pale ambapo atakuwa ni mwenye kujitenga mbali na dini zote isiyokuwa Uislamu na mpaka aseme kwa yakini ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah`. Endapo atajua na akakataa kutamka licha ya kwamba anao uwezo wa kufanya hivo, basi anazingatiwa ni kafiri.

[1] Ahmad (1/65). Ni yenye cheni ya wapokezi Swahiyh kwa mujibu wa Ahmad Shaakir.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/306)
  • Imechapishwa: 06/11/2020