Bado anaitwa ubini wa mumewe wa kitambo


Swali: Muulizaji mwanamke kutoka UK anasema; nimezaliwa katika familia ambayo si ya Kiislamu na wazazi wangu hawakuoana, halafu nikaolewa na mume mwingine na nikajiita kwa ubini wake [huyo baba mdogo]. Je, ni wajibu kwangu kubadilisha jina langu kwa kuwa unasibisho wa mwanamme huyu si sahihi kwa kuzingatia ya kwamba kubadilisha jina kwetu inaweza kutusababishia madhara?

Jibu: Ni wajibu kwako kubadilisha jina. Haijuzu kwako kujiita ubini kwa mtu ambaye si baba yako. Kalaaniwa yule ajiitaye kwa ubini ambao si wa baba yake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ

“Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.” (33:05)

Ni wajibu kwako kubadilisha jina lako. Usibaki hali ya kuwa ni mwenye kunasibishwa kwa mwanamme ambaye si baba yako. Na uwe mwenye subira kwa yatayokusibu katika madhara na wewe utakuwa mwenye kupewa ujira – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13840
  • Imechapishwa: 04/07/2021