Badala ya kwenda sujuud ya kisomo ameenda katika Rukuu´

Swali: Ni kipi kinachompasa mwanamke pindi imamu anaposujudu sijda ya kisomo na yeye mwanamke akarukuu. Je, analazimika kuleta sijda ya kusahau au afanye nini?

Jibu: Imamu akisujudu sijda ya kisomo asujudu pamoja naye na asirukuu. Lakini akirukuu kwa kusahau hakuna kinachomlazimu. Ikiwa amefanya hivo sehemu ya mwisho ya swalah yake na amepitwa na baadhi ya Rak´ah, basi anatakiwa kusujudu sijda ya kusahau kabla ya salamu. Lakini kama alianza na imamu mwanzoni mwa swalah basi yeye imamu ndiye mwenye kumbebea jukumu hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Khaatam-ul-Mursaliyn https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-10/lqa-mftoh-godian.mp3
  • Imechapishwa: 26/09/2022