Babamkwe hataki msichana wake asafiri na mume wake

Swali: Mimi nina wake wawili katika mji wa ´Asiyr na baba zao wanawakataza kusafiri pamoja naye na anakuwa mbali nao kwa miezi mingi. Je, ninapata dhambi?

Jibu: Ikiwa alimuwekea sharti kabla ya ndoa kutosafiri nao basi baba zao wako na haki ya kuwazuia kusafiri nao midhali wenyewe hawajapenda kusafiri pamoja naye. Wakipenda wenyewe kusafiri pamoja naye basi itakuwa ni haramu kwa baba zao kuwazuia. Kwa sababu wake wawili hao ndio wenye haki. Ikiwa hakumuwekea sharti hiyo basi mume ni mwenye kummiliki mke wake. Akisafiri na akaomba kusafiri pamoja na wakeze basi ni lazima kwao wawili hao kusafiri pamoja naye na hapo itakuwa ni haramu kwao na kwa baba zao kuwazuia. Wakikataa au baba zao wakawazuia basi hakuna neno akisafiri na akachelewa kuwajia. Kwa sababu ukweli wa mambo uasi umetokamana na wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (17) http://binothaimeen.net/content/6821
  • Imechapishwa: 17/03/2021