Baba yake Mtume (´alayhis-Salaam) alikufa mshirikina


Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kwamba mama yake Mtume na baba yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) sio waumini wala makafiri, bali ni katika…

Jibu: Haya ni maneno yasiyokuwa na maana. Baba yake na Mtume yuko katika dini ya watu wake. Dini ya watu wake ilikuwa ipi? Shirki. Hivyo ni mshirikina na ni katika watu wa Motoni. Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia mtu ambaye alimuuliza: “Yuko wapi baba yangu?” Akasema: “Baba yako yuko Motoni”. Mtu yule akajihisi kama kuumia ndani ya moyo wake. Hivyo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Baba yangu na baba yako wote wako Motoni”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-27.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014