Baba kumtalikia mtoto wake


Swali: Je, inajuzu kwa baba kumtaliki mke wa mtoto wake kukiwepo sababu?

Jibu: Haijuzu isipokuwa tu ikiwa baba yuko na utawala juu yake, au ni mdogo au ni mwendawazimu. Ikiwa ana utawala juu yake, hapo anaweza kumtalikia. Au mtoto ndiye akawa amemwakilisha baba kwa hilo. Ikiwa ni mtoto ndiye kamwakilisha baba kuwa anaweza kumtaliki mke wake, hakuna ubaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10011
  • Imechapishwa: 07/03/2018