Baba kumtafutia binti yake mwanaume mzuri

Walii kumtafutia mwanamke mwanaume mzuri ni Sunnah. ‘Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘anh) alimuuliza ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘anh) kama anataka kumuoa binti yake Hafswah. Akakataa. Kisha akamuuliza Abu Bakr kama anataka kumuoa, lakini na yeye akawa amekataa. Baada ya hapo akamuomba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kumuoa. Baada ya yeye (´Uthmaan) kufanya hivyo, Abu Bakr akamwambia ´Umar ya kwamba alimkataa binti yake tu kwa sababu alikuwa amesikia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) anamtaja Hafswah. Alikataa kwa ajili ya heshima kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Hivyo ni vizuri mtu kumtambulisha binti yake kwa watu wazuri. Ndani yake hakuna upunguzu wowote, bali ni jambo bora.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (20)
  • Imechapishwa: 22/09/2020