Swali: Ipi hukumu ya baba ambaye hataki kuwaozesha mabinti zake kwa ajili ya riziki zao?

Jibu: Huchukuliwa kuwa ni dhalimu. Allaah hawapendi madhalimu. Allaah amesema:

وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا

”Wenye kudhulumu amewaandalia adhabu iliyo chungu.” (76:31)

Riziki yao iko kwa Allaah. Akimuozesha binti yake riziki yake iko kwa Allaah. Ajitahidi kumuozesha kwa mwanamume mwema ambaye atamsaidia katika dini na dunia yake. Haijuzu kwake kumkatalia kwa kitu alichomhalalishia Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4706
  • Imechapishwa: 22/09/2020