Baba ataka kumuozesha msichana ambaye ni mgonjwa


Swali: Kuna msichana ambaye ni mgonjwa na anatumia madawa na hataki maisha ya ndoa jambo ambalo ndio ilikuwa sababu ya kutalikiwa sababu ya maradhi hayo. Je, inajuzu kwa msimamizi wake kuwaambia watu hastahiki kuolewa?

Jibu: Msimamizi wake awe na subira kwake mpaka yatapomuondoka maradhi hayo kisha ndio amuozeshe. Ama kumuozesha ilihali bado yuko katika hali hii sio jambo liko katika manufaa yake. Awe na subira kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13389
  • Imechapishwa: 25/04/2018