Baba anawataka watoto kumkata ami yao

Swali: Kulitokea ugomvi kati ya baba yangu na ami yangu. Kukatokea kati yao mivutano. Baba yetu akatuamrisha kutomtolea salamu ami yetu na kumkata. Je, hili linaingia katika kukata udugu?

Jibu: Ndio, haya yanaingia katika kukata udugu. Baba asitiiwe katika hayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Ni wajibu kwa watoto wa baba huyu kumsalimia ami yao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 03/01/2018