Baba ameacha wasia atolewe swadaqah kila mwaka nisfu Sha´baan

Swali: Baba yangu aliniusia maishani mwangu kutoa swadaqah kwa kiasi na uwezo wangu usiku wa nisfu Sha´baan kila mwaka. Nilikuwa nikifanya hivo mpaka hii leo pamoja na kuwa baadhi ya watu wananikataza kufanya hivo na kunambia kuwa inaweza kuwa haijuzu. Je, swadaqah hii usiku wa nisfu Sha´baan inajuzu kutokana na wasia wa baba yangu au haijuzu?

Jibu: Kukhusisha swadaqah hii nisfu Sha´baan kila mwaka ni Bid´ah isiyojuzu hata kama baba yako amekuusia kufanya hivo. Ni juu yako kutekeleza swadaqah hii lakini usikhusishe kwa kuitoa nisfu Sha´baan. Itoe kila mwaka katika mwezi wowote ndani ya mwaka pasi na kukhusisha mwezi maalum. Ingawa bora zaidi uitoe katika Ramadhaan.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (3/52)
  • Imechapishwa: 23/08/2020