Baadhi Ya Tofauti Kati Ya Salafiyyah Na ISIS


Swali: Vipi tutajua ni kundi lipi lililookoka (Firqat-un-Naajiyah) wakati kuna mapote mengi leo?
Jibu: Kundi lililookoka alama zake ziko wazi. Ni wale wenye kushikamana na yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Wanaipa kipaumbele Sunnah juu ya kila kitu. Hawana mapenzi kwa Ahl-ul-Bid´ah. Hawafanyi Bid´ah. Wanawapiga Radd Ahl-ul-Bid´ah. Wanatilia juhudi katika kutekeleza Sunnah kwa aina zake zote. Alama zake ziko wazi ikiwa ni pamoja na kupenda Sunnah, Ahl-us-Sunnah na kuzitendea kazi Sunnah.

Ama kuhusiana na madai, ni mengi. Kuna watu leo wanaosema kuwa ni Ahl-us-Sunnah na wakati wanawaua Ahl-us-Sunnah. Wanadanganya. Kwa mfano wa ISIS. Mwenye kusema kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah na kuhalalisha damu ya Waislamu sio katika Ahl-us-Sunnah. Mwenye kusema kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah na kuziweke taawili Sifa za Allaah (´Azza wa Jalla) sio katika Ahl-us-Sunnah. Mwenye kusema kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah na ana fikra za ki-Irjaa´ sio katika Ahl-us-Sunnah. Wana alama zilizo wazi zinazowapambanua.

Anayeita katika kufuata Sunnah na wanachuoni Rabbaaniyyuun[1] na kuwa elimu ichukuliwe kutoka kwao na kwamba watu waende katika duruus zao na kusoma kwao ndio Ahl-us-Sunnah hata kama watakuwa wachache.

[1] Tazama http://www.wanachuoni.com/content/maana-ya-wanachuoni-rabbaaniyyuun

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=145877w
  • Imechapishwa: 07/11/2016