Baadhi ya misikiti inachelewesha swalah ya ijumaa na mingine inaitanguliza

Swali: Katika baadhi ya miji kuna misikiti ambayo kunaswaliwa ndani yake swalah ya ijumaa katika ule wakati wake wa kwanza baada ya jua kupinduka na misikiti mingine wanaswali swalah ya ijumaa muda kidogo kabla ya ´Aswr. Wanafanya hivo hivo kwa sababu siku ya ijumaa ni siku ya kazi huko na sio siku ya mapumziko. Kwa hivyo wanaigawa swalah ya ijumaa katika nyakati mbili kwa ajili ya kuwawepesishia watu wote kudiriki na kwenda katika swalah ya ijumaa. Je, kitendo hichi kimewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Ikiwa ni katika misikiti mbalimbali hakuna neno. Ama ikiwa hayo yanafanywa katika msikiti mmoja hapana. Kusifanywe hayo. Ni sawa baadhi ya misikiti inachelewesha swalah na misikiti mingine ikatanguliza kwa ajili ya manufaa ya watu midhali inaswaliwa ndani ya wakati wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-26-10-1434.mp3
  • Imechapishwa: 21/10/2017