Swali: Baadhi ya watu wakati wa likizo wanaenda nje ya Saudi Arabia kwa haja au pasi na haja. Ni mamoja katika nchi ya kiarabu zilizoharibika au kwenda katika nchi ya kimagharibi ya kikafiri. Wanaponasihiwa wasisafiri wanasema kwamba ni katika burudani iliyoruhusiwa, kwamba vitu hapa kwetu vina bei na mfano wa hayo. Ni kipi kinachoniwajibikia juu yake ikiwa ni ndugu yangu? Ni zipi nasaha zako kwako yeye na watu mfano wake?

Jibu: Nasaha zangu kwa ndugu zangu waislamu ni kwamba wasizibadilishe neema za Allaah kufuru. Sisi – himdi zote zinarejea kwa Allaah – tuko katika kheri kama amani na maisha mazuri. Tunaposikia taarifa ya khabari, vita kati ya watu, umasikini na khofu, basi tunaona kuwa tuko ndani ya neema. Ni vipi tutaikabili neema hii kwa kuikufuru?

Kusafiri kwenda katika mji wa kikafiri au kwenda katika mji wa burudani, kama anavosema muulizaji, ni jambo la khatari juu ya ´Aqiydah, tabia na khatari juu ya familia. Kwa sababu mtu akiona kufuru huko basi hatoikimbia kama angelivyokimbia kabla ya kuiona. Akiona kufuru, akasikia nyimbo na turumbeta za mayahudi basi ukafiri atauona mwepesi moyoni mwake, jambo ambalo ni kasoro katika ´Aqiydah. Kadhalika ataona huko ataona nyumba za wamalaya, uzinzi, ushoga na unywaji pombe, mambo ambayo yanaathiri katika tabia. Vivyo hivyo wale watoto katika familia. Watoto hawasahau sura waliyoiona utotoni mwao. Sura hii itarudi kichwani mwake hata huko baadaye. Matokeo yake mwanaume huyu anakuwa amefanya vibaya juu yake mwenyewe na juu ya familia yake. Jambo jengine ni kwamba kitendo hichi kina kukuza uchumi wa makafiri. Jengine pia ni kwamba unadhoofisha uchumi wa nchini. Kwa sababu shilingi moja inayotoka hapa na kwenda huko ina maana kwamba imepungua na kukuza uchumi wa nchi nchi nyingine. Halafu isitoshe makafiri hawa wanafurahi sana pindi wanapowaona watu wameifanya nchi yao kuwa kama makazi. Yote haya ni madhara. Mwenye busara, sembuse muumini, hafanyi kitu kama hicho. Tunamuomba Allaah awaongoze vijana wetu katika yaliyo na kheri juu ya dini na dunia yetu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1265
  • Imechapishwa: 05/10/2019