Baadhi ya madhara ambayo maandamano yamesababisha


Swali: Mwenye kusema kuwa maandamano yanajuzu mtu atahadharishe watu naye au ni masuala ya Ijtihaad?

Jibu: Maandamano hayajuzu kwa hali yoyote. Nyinyi mmeona maandamano kwa macho yenu, tazamani uharibifu, maangamivu, nafsi ngapi yamesababisha kutoweka, watoto na wanawake, majumba mangapi na miji yameangusha? Maandamano hayafai. Dawa sio kwa kutumia maadamano. Dawa ni kwa kutumia njia za Kishari´ah ili kufikia makusudio. Hili linakuwa kupitia mikono ya wanachuoni na waonao mbali. Haliwi kupitia mikono ya wasiokuwa na elimu au mtu ni mtu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls--14340327.MP3
  • Imechapishwa: 05/09/2020