Baadhi ya faida za kuoa

Swali: Kuna watu wanaocha kuoa kwa ajili ya kuipa nyongo dunia. Je, huyu anazingatiwa ni mzushi au ni mwenye kwenda kinyume na Shari´ah?

Jibu: Huyu ni mwenye kwenda kinyume na Shari´ah. Kuoa kunatakikana. Kitu cha kwanza kunamuhifadhi mtu na tupu kutokamana na haramu. Pili ndani yake kunamfanya mtu kupata watoto. Tatu kunampa mtu usimamizi juu ya wanawake:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake.”[1]

Katika kuoa kuna kheri nyingi.

[1] 04:34

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (79) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-9-2-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 05/03/2018