Baadhi ya Adhkaar zilizopokelewa katika Sujuud

Swali: Kipi niseme katika Sujuud na Rukuu´?

Jibu: Kilichowekwa katika kwenye Sujuud Shari´ah ni wewe kusema:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

mara tatu.

Kwenye Sujuud useme:

سبحان ربي الأعلى

“Ametakasika Mola wangu Aliye juu.”

mara tatu au zaidi ya hapo.

Idadi ya lazima ni mara moja kwa zote mbili kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni.

Imependekezwa pamoja na haya aseme katika Rukuu´ na Sujuud:

سبحانك اللهم ربنا وبحمدك اللهم اغفر لي

“Ametakasika, Mola wetu, himdi zote ni Zake. Ee Allaah! Nisamehe.”

Imependekezwa kusema hivo na mwanamme na mwanamke, katika swalah za faradhi na swalah za sunnah. Vilevile imependekezwa akaomba du´aa kwa wingi katika Sujuud. Imependekezwa katika Sujuud na Rukuu´ akasema:

سبوح قدوس رب الملائكة والروح

“Umetakasika sana kutokamana na mapungufu na uchafu; Mola wa Malaika na roho!”

سبحان ذي الجبروت والملكوت والكبرياء والعظمة

“Ametakasika kutokamana na mapungufu Mwenye utawala, ufalme, ukubwa na utukufu.”

Du´aa hii imependekezwa katika Rukuu´ na Sujuud.

Du´aa zinazombwa katika Sujuud peke yake. Ama Rukuu´ ni sehemu ya kumtukuza Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ama Rukuu´ mtukuzeni Mola. Ama Sujuud jitahidini katika du´aa kuna matarajio mkubwa mkaitikiwa.”

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mahali mja anapokuwa karibu zaidi na Mola Wake ni pale anapokuwa amesujudu. Hivyo kithirisheni kuomba du´aa.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9532/اذكار-السجود-والركوع
  • Imechapishwa: 01/05/2020