Baada ya kutwahirika akakutana na mumewe, damu imejitokeza tena

Swali: Mwanamke alikuwa na hedhi na baada ya masaa sita akatwahirika. Na baada ya mume wake kumjamii, hedhi ikarudi. Afanye nini?

Jibu: Ikiwa siku zake za ada ni sita kwa mfano, na siku sita hizo zikapita, asijali kwa hichi kilichodhiri. Isipokuwa tu ikiwa jambo hili litakariri, hapo kutatazamwa. Au itatazamwa vile vile damu yake ni nyingi au ndogo, ikiwa ni damu ndogo haidhuru. Na ikiwa ni damu nyingi, atachukulia damu ya siku zile kuwa ni damu ya hedhi. Haruhusiwi kuswali wala kufunga. Na kwa kutumia fursa hii, nimeambiwa kuwa baadhi ya wahubiri Hudaydah wametusemea uongo na kusema kuwa mimi naamrisha mwanamke kulipa Swalah zake na asilipe Swawm. Huu ni uongo. Mikanda ipo inayotolea ushahidi hilo. Anadai kuwa kaambiwa na watu waaminifu. Ni watu gani waaminifu ambao wamekwambia hivyo wewe masikini?

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?sec_id=15
  • Imechapishwa: 07/03/2018