Baada ya ´Iysaa Nabii mwingine zaidi ya Muhammad?

Swali: Katika maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ

… kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake ´Ahmad`.” (61:06)

ni dalili yenye nguvu inayofahamisha kwamba hakuna baada ya ´Iysaa isipokuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam)?

Jibu: Bila shaka. Aayah hiyo ni miongoni mwa dalili. Vivyo hivyo maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakiki mimi ndiye mwenye haki zaidi kwa ´Iysaa mwana wa Maryam na kwamba hakuna kati yangu mimi na yeye Nabii mwingine.”

Hii ni dalili juu ya ubatilifu wa Hadiyth ambayo ndani yake yumo Khaalid bin Sinaan kwamba baada ya ´Iysaa atakuja Nabii mwingine. Hadiyth hiyo si Swahiyh.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
  • Imechapishwa: 22/05/2020