Baada ya imamu kuingia ndani ya swalah amekumbuka kuwa hana wudhuu´

Swali: Imamu akileta Takbiyrat-ul-Ihraam kisha papohapo akakumbuka kuwa hana wudhuu´. Akarudi nyuma na akamtanguliza yule ambaye yuko nyuma yake ambapo mtu huyu hakuleta Takbiyrat-ul-Ihraam. Wale wengine walioko pembezoni mwake ni wadogo na hakuwatanguliza kwa sababu bado wako masomoni. Ni kipi kinachomuwajibikia?

Jibu: Mtu ameenda kuwaswalisha watu na akakumbuka kuwa hana wudhuu´, tunasema: ni wajibu kwake kuondoka na wala asione haya. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) haoni haya juu ya haki. Nyuma yake kukiwa ambaye anaweza kuendelea kuwaswalisha watu hawa, basi amvute na kumtanguliza na amwambie awakamilishie swalah yao. Ikiwa nyuma yake hakuna ambaye anasilihi kuwa imamu, basi awaambie kila mmoja aswali kivyake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (64) http://binothaimeen.net/content/1456
  • Imechapishwa: 08/01/2020