Swali: Watu wengi wa kawaida wanasema “Allaah Yuko kila mahala”. Ninapowawekea wazi ya kwamba msemo huo ni kufuru, wanasema “Mimi sijui hilo na mtu anachukuliwa kutokana na nia yake”. Niseme nini?

Jibu: Sio jambo zuri. Mwambie “Alhamduli Allaah, wewe kwa hivi sasa umejua haki na usiseme tena hivo mara nyingine”. Akitekeleza, Alhamduli Allaah, anapewa udhuru kwa ujinga wake, na ikiwa hakutekeleza inakuwa anafanyia kusudi. Hivyo anakuwa ni katika Huluuliyyuun.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar
  • Imechapishwa: 14/11/2014