Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kusema:

أعوذ بالله من الشيطان الرجيم

“A´udhubi Allaahi min as-Shaytwaan ar-Rajiym”

wakati wa kupiga miayo?

Jibu: Hapana. ´Awwaam ndio wenye kusema hivo. Lililowekwa katika Shari´ah ni yule mwenye kupiga miayo ajizuie kiasi na anavyoweza. Ikiwa hatoweza kufanya hivo aweke mkono au kitu kingine kwenye mdomo wake. Apige miayo kwa kufungua kinywa na wala asitoe sauti. Ajizuie kiasi na anavyoweza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-13.mp3
  • Imechapishwa: 12/06/2018