´Awwaam kufanya Taqliyd madhehebu mane

Swali: Ni jambo la kupindukia kufuata kipofu moja katika madhehebu mane?

Jibu: Hapana. Mtu ambaye si msomi na ambaye anaanza sasa hawezi jengine zaidi ya kufuata kipofu. Vinginevyo afanye nini? Afanye Ijtihaad mwenyewe? Hana uwezo wa kufanya Ijtihaad. Awafuate wanachuoni. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Waulizeni watu wenye kumbukumbu Ukumbusho ikiwa hamjui.” (16:43)

Kwa nini wawaulize? Ili wafuate yale wanayoyasema. Kufuata kichwa mchunga inakuwa kwa sababu ya dharurah na haja. Ambaye hana uwezo wa kutafiti dalili na kuonelea usawa awafuate wanachuoni:

فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

“Waulizeni watu wenye kumbukumbu Ukumbusho ikiwa hamjui.” (16:43)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%20-%2017-%2010-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017