Atiiwe mtu ambaye anaiambia familia yake wasimwamshe kwa ajili ya swalah?

Swali 16: Ni ipi hukumu ya mtu anayekusudia kuiambia familia yake wasimwamshe kwa ajili ya kuswali ilihali anajua kuwa punde tu  kutaadhiniwa kwa ajili ya swalah?

Jibu: Ni wajibu kumuasi, wamwamshe, wamnasihi na wamwelekeze katika kheri kwa kuwambia:

“Mche Allaah! Amka uswali!”

Wasimtii katika maasi. Lau baba au mama yako atakwambia usimtaje Allaah utawatii?

Iwapo ataacha swalah kwa kukusudia mpaka ukatoka wakati wake anakufuru kwa maoni yaliyo na nguvu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baina ya mtu na kufuru na shirki ni kuacha swalah.”[1]

Ama wanachuoni wengi wanaonelea kuwa hakufuru midhali anaamini kuwa ni wajibu lakini ameacha kwa sababu ya uvivu.

[1] Muslim (82)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 33
  • Imechapishwa: 04/10/2018